kundi la ISISi kutangaza taifa la kiislamu.
Nchini Iraq hali inaendelea
kuzorota, raia wakiendela kukimbia mapigano .
Sasa wapiganaji wa kiislam wa Kundi la iSIS wamesema kuwa wanataka kuweka utawala wao baada ya kudhibiti maeneo ya Iraq na Syria.
Msemaji wa wanamgambo hao wa
kiislamu wa ISIS ametangaza kuwa wataunganisha ardhi wanazozidhibiti
walizoziteka kutoka Iraq na Syria ndio waunde eneo moja wanalolitaja kama
'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu.
Kama vile ilivyotolewa taarifa ya
Shami ndivyo ilivyotangazwa kauli ya Shaykh Abu Muhammad al-Adnani, kupitia
mtandao wa You Tube.
ISIS wameteka maeneo Iraq na Syria.
Serikali ya Iraq ina wakati mgumu kukabiliana nao.
Ameendelea kusema eneo hilo
litajumuisha tangu Aleppo huko Syria hadi Diyala mashariki mwa Iraq.
Na kufuatia hali hiyo msemaji huyo
amefafanua kwamba sasa kundi hilo badala ya kuwa na kujulikana kwa jina la
ufupi ISIS na the Levant sasa watajiita tu "the Islamic State" Taifa
la kiislam.
Kundi hilo pia limesema limemteua
kiongozi wao -- Abu Bakr al-Baghdadi -- kama 'Caliph', wakidai ndio kiongozi wa
waslamu wote.
Haya yote yanatangazwa baada ya
kundi hilo la Isis kupata mafanikio makubwa katika vita vivyo.
Wakati huo huo Serikali ya Iraqi
imesema vikosi vyake vimepiga hatua kuelekea Tikrit, mji wa kazkazini mwa nchi
hiyo uliotekwa na wanamgambo hao wa kiislamu zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msemaji wa jeshi la Iraqi Luteni
jenerali Qassim al-Moussawi amesema jeshi lao liko katika awamu ya kwanza ya
mapigano hayo ya tangu alhamisi.
Televisheni ya kitaifa ilionesha
helicopters zikishambulia maeneo kadhaa huko jangwani lakini hamna ushahidi
kamili wa kuaminika kwamba wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuingia mjini.
Waasi hao wametega mabomu kando
kando mwa barabara kuu kujaribu kuzuia vikosi vya serikali.
Hata hivyo mwandishi wa BBC aliyeko
Baghdad amesema hii ndio hatua ya kwanza thabiti iliyowahi kuchukuliwa na
serikali dhidi ya ISIS tangu waasi hao walipoanza kushambulia na kuyateka
maeneo ya nchi hiyo kwa kasi iliyowashangaza wengi.
No comments