R Kelly akwepa maswali, ni kuhusu mtoto wake kubadilisha jinsia
Mwanamziki
wa Marekani Robert Kelly maarufu kama R.kelly amekataa kujibu maswali
yanayomhusu mtoto wake wa kike Jaya kubadilisha jinsia.kuwa wa kiume R Kelly
amekuwa akikwepa kujibu maswali hayo juu ya hatua ya mtoto wake mwenye umri wa
miaka 13 aliyotangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa amebadilisha jinsia yake
na kuwa wa kiume akijiita Jay Kelly.Mwanamuziki huyo maarufu kutoka nchini
Marekani amesema kuwa hatopenda kulizungumzia suala hilo la mtoto wake
kujibadili jinsia na kuongeza kuwa hata kama kuna ukweli wowote hatovipa vyombo
vya habari uhuru wa kuzungumzia.R Kelly ameongeza kuwa ni vyema watu wakaamini
wanachokiona kwa macho kuliko wanachosikia kwani hata yeye amesikia juu ya
suala hilo lakini si kweliR Kelly amebarikiwa kuwa na watoto wengine wawili
Joann Kelly na Junior Robert Kelly aliozaa na mke wake wa zamani Andrea Kelly.
No comments