ads

Breaking News

Aibu! Mke amwangushia kichapo cha Mbwa mwizi hawara wa Mumewe Usiku huko UKONGA

KUNA matukio ambayo kama binadamu yasikie kwa wengine tu lakini yasikutokee wewe! Kama hili la mkazi wa Ukonga –Mzambarauni, Dar, Paulo Ndulu ambapo mkesha wa kuamkia Sikukuu ya Sabasaba, alijikuta katika wakati mgumu pale alipoingia kibaruani kuamua ngumi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha aliyedaiwa kuwa ni hawara yake,


Bw. Paulo Ndulu  akijaribu kuamua ugomvi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha (mwenye shati nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.
Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuamua ugomvi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha (mwenye shati nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.


...Iilikuwa ni soo la kufa mtu.
…Iilikuwa ni soo la kufa mtu.

  USIKU

Siku ya tukio, majira ya saa nane usiku,  maeno ya Ukonga jijini Dar  timbwili zito sana kutoka kwenye nyumba ya Ndulu huku majirani kibao wakiziba mtaa kushuhudia.
Bw. Paulo Ndulu akiendelea kuamua ugomvi huo.
Bw. Paulo Ndulu akiendelea kuamua ugomvi huo.
 sekeseke hilo na kugundua kuwa, ndani ya nyumba ya Ndulu kulikuwa na kasheshe zito la nguo kuchanika kati ya wanawakwe wawili ambapo majirani walisema mmoja ni mke, mwingine hawara, kisa?


...Mara majirani nao walishuhudia ugomvi uliokuwa ukiendelea kwa kupiga chabo dirishani.
…Mara majirani nao walishuhudia ugomvi uliokuwa ukiendelea kwa kupiga chabo dirishani.

MSIKIE JIRANI

“Mke aliaga anasafiri, mume akaingiza mwanamke mwingine, sasa kumbe mke hakusafiri kikweli, alimdanganya mumewe baada ya kujua kuna mwanamke atakuja,” alisema jirani mmoja huku akilalamika kwamba, amepika daku linapoa kwa sababu ya kushuhudia filamu hiyo ya bure.
Ilidaiwa kuwa, Anitha alikuwa katika wakati mgumu baada ya mumewe kuwa na tabia ya kumwingiza mwanamke huyo ndani na kumwambia yeye akakae mahali anywe soda au aende kwao mpaka mgeni wake atakapoondoka ndipo arudi.


Bw. Paulo Ndulu akizidi kumsihi mkewe apunguze munkari.
Bw. Paulo Ndulu akizidi kumsihi mkewe apunguze munkari.

ALIJIFICHA

Siku ya tukio, kwa mujibu wa mashuhuda, Anitha alipobaini ujio wa mgeni huyo (Elizabeth) alijifanya anakwenda Kimanzichana, Kisarawe, Pwani lakini uhalisia alikwenda kujificha nyumba ya jirani huku akiweka wapambe wampigie chabo nyendo za mumewe kwa usiku huo kwa sababu alikuwa amechoshwa na uonevu wa kutakiwa kwenda kukaa mahali.


Bi. Anitha Mapunda (mke wa Paul Ndulu) akiwa na gadhabu kubwa.
Bi. Anitha Mapunda (mke wa Paul Ndulu) akiwa na gadhabu kubwa.

MUME ARUDI, HAWARA ATINGA

Chanzo kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani hapo. Muda si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia nyumbani hapo na Ndulu alitoka kumpokea.
Makamanda wa OFM wakimdhibiti hawara alipotaka kukimbia.
Makamanda wa OFM wakimdhibiti hawara alipotaka kukimbia.

WAPAMBE WANYAKUA VIATU VYA ELIZABETH

Jirani huyo alizidi kusema kuwa, wakati Eliza akizama ndani Ndulu, alivua viatu na kuviacha nje ya mlango. Wapambe wakavichukua na kwenda kumuonesha Anitha akiwa mafichoni ili kumthibitishia kuwa tayari mumewe alikuwa na kifaa ndani.


...Hawara huyo (Elizabeth Chacha) akikalishwa chini ili wayamalize kiutu uzima.
…Hawara huyo (Elizabeth Chacha) akikalishwa chini ili wayamalize kiutu uzima.
Baada ya kuoneshwa viatu hivyo, Anitha alichanganyikiwa na kutoka kwenda nyumbani kwake ambapo aliingia na kusababisha varangati hilo la aina yake lililodumu kwa karibu dakika ishirini mpaka  askari wa kulida doria usiku walitinga eneo la tukio.
Bi. Elizabeth Chacha akisikiliza kwa hofu uamuzi uliochukuliwa.
Bi. Elizabeth Chacha akisikiliza kwa hofu uamuzi uliochukuliwa.

MJUMBE ASHIRIKISHWA

Ili kuweka sawa mambo ya kisheria, maafande hao wenye maadili ya kazi walikwenda hadi kwa Mjumbe wa Shina Namba 29, Mama Urio ambaye waliongozana naye mpaka kwenye eneo lenye kizaazaa.Hata hivyo, polisi na mjume huyo walimkuta Anitha ameshamvaa mbaya wake huyo huku akimtupia maneno yenye lawama na shutuma nzitonzito kwamba anamvunjia nyumba yake.


...Majirani walifika eneo la tukio na kushuhudia mkasa huo.
…Majirani walifika eneo la tukio na kushuhudia mkasa huo.

WATU DIRISHANI WEWEEE!

Ndulu mbali ya kuchoka hoi kufuatia kazi nzito na kumdhibiti mkewe asiendelee kuzichapa na Eliza, pia alikuwa na kazi nyingine ya kugombana na majirani ‘wambeya’ walijaa dirishani kwa nje wakimporomoshea maneno yenye kuudhi.


...Wananchi wakiendelea kujionea laivu yaliyojiri.
…Wananchi wakiendelea kujionea laivu yaliyojiri.

UTETEZI WA NDULU

Baada ya hali ya hewa kutulia, polisi walimuhoji Ndulu kuhusu sakata hilo, alikiri kuishi na Anitha kwa zaidi ya miaka minne lakini alimkana kuwa si mkewe kwa kuwa yeye ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki na hakuwahi kufunga naye ndoa.


Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuwafukuza mashuhuda wa tukio hilo la aibu.
Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuwafukuza mashuhuda wa tukio hilo la aibu.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndulu ulipingwa vikali na mjumbe wa nyumba kumi na polisi ambapo walimwambia kisheria mwanaume na mwanamke wakiishi ndani ya nyumba kwa muda huo tayari ni mkewe.
Wakasema kwa hiyo kitendo cha kumpelekea mwanamke mwingine ndani ni kutafuta machafuko kwa makusudi.


Bw. Paulo Ndulu akijitetea kuhusu uhusiano wake na hawara huyo.
Bw. Paulo Ndulu akijitetea kuhusu uhusiano wake na hawara huyo.

ELIZABETH SASA

Wakati wote wa sakata, Elizabeth alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema amekoma kwani Ndulu alimwambia kuwa haishi na mwanamke baada ya kuachana na Anitha muda mrefu kwa sababu za ugumba.


Bi. Elizabeth Chacha akiondoka pekupeku eneo la tukio.
Bi. Elizabeth Chacha akiondoka pekupeku eneo la tukio.
“Mimi aliniambia haishi na mwanamke na nilimuuliza sana kuhusu hili naye akanithibitishia kuwa ni msela lakini hata hivyo machale yalikuwa yakinicheza muda wote, namuomba radhi mwanamke mwenzangu jamani,” alisema Eliza.


Bi. Elizabeth Chacha akiondoka pekupeku eneo la tukio.
Bi. Elizabeth Chacha akiondoka pekupeku eneo la tukio.

MWISHO WA SAKATA

Hatima ya sakata hilo, Elizabeth alitakiwa kurudi kwao, Ubungo -Maziwa jijini Dar na Anitha alishauriwa kwenda kulala kwa kaka yake anayeishi jirani na eneo hilo chini ya usimamizi wa mjumbe.

ANITHA MWENYEWE

Akizungumza  baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za  karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata Eliza

No comments