ads

Breaking News

Chukua hiyo: Gari hili linaweza kutumika miaka 100 bila kuongezwa mafuta (Video




Moja kati ya mambo ambayo mtu wa anayafikiria kabla
hajanunua gari ni kiasi cha mafuta kinachotumiwa na gari hilo. Lakini
ukiwa na gari hili… unaweza usifikirie kabisa kuhusu mafuta huku
ukilitumia kama kawaida kwa zaidi ya miaka 100.

Wataalam wa masuala ya magari wameeleza kuwa endapo gari linalotumia
‘Thorium’ litaanza kufanya kazi litakuwa gari ambalo linaweza kutumika
kwa zaidi ya miaka 100 bila kuongezwa mafuta.

Kwa maana hiyo Thorium itakuwa na uwezo wa kudumu hata zaidi ya maisha ya mtumiaji wa gari hilo.

Kampuni ya Laser Power tayari imeshatengeneza idea ya kutumia Thorium
katika engine za magari  ambapo wataitumia kitaalam kuchemsha maji na
kuwa chanzo cha nguvu ya kuendesha gari.

Hata hivyo, CEO wa Laser Power System, Dr. Charles Sevens aliiambia
Mashable kuwa engine za Thorium hazitaweza kuwa kwenye magari hivi
karibu kwa kuwa watengenezaji wa magari hawataki kuzinunua.

Cars are not our primary interest. The automakers don’t want to buy them.” Alisema Dr Charles Stevens.







Alisema makampuni mengi ya magari yanataka kutengeneza pesa zaidi kwa
kutumia engines za gas na kwamba itawachukua miongo kadhaa kukubali na
kuanza kutmia teknolojia ya Thorium.

Endapo gari hili litafanikiwa kuingia sokoni na kununuliwa na watu
wengi miaka ijayo, itakuwa hatari kwa biashara ya mafuta hasa kwa wale
wanaotegemea magari pekee kufanya mauzo.

No comments