GARI LA MSANII MAARUFU WA BONGO MOVIE LAKAMATWA KWA UJAMBAZI
GARI la
muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na
Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi
linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka
huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajiliT 360 BAJ, lilikutwa
likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif
Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSCiliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Inadawa kuwa muda mfupi baada ya
kukamatwa, Dude alitokea Polisi na kulitambua gari lake, lakini maelezo
yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo kumshikilia katika kituo kidogo cha
Polisi Mabatini hadi kesho yake alipodhaminiwa. Muonekano wa gari hilo kwa nyuma.
Waandishi wetu walifanya jitihada za
kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo, lakini aliwataka kufuatilia
jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema suala hilo lipo mikononi
mwao.
Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI
No comments