Mifuko ya plastiki inayoaminika kuwa na mabaki ya viungo na mabaki ya miili ya binadamu Dar es Salaam
Mifuko ya plastiki inayoaminika kuwa na mabaki ya viungo na mabaki ya miili ya binadamu ikiwa imetelekezwa kwenye eneo la machimbo Mbweni Mpiji Magohe, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam janaMifuko ambayo imesheheni mabaki ya kile kilichoelezwa kuwa ni mabaki ya miili ya binadamu ambayo ilitupwa na kugundulika mapema leo kwenye eneo lamachimbo Mbweni Mpiji Magohe, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
Kwa
mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe
amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo
vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.
Mtu
mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa
akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
SASA Habari zimethibitisha kwamba masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa maeneo ya Bunju yametoka chuo cha udaktari IMTU kilichopo Mbezi baada ya wanafunzi kumaliza kutumia kwa mazoezi. Viungo hivi vilitupwa baada ya Kukosa pesa za kuteketeza kwenye tanuri maalum.
No comments