ads

Breaking News

Ratiba ya Serengeti Fiesta 2014 imetoka,Hii hapa.

fiestaa
Fiesta ni tamasha linalowakutanisha wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva kwenye msimu wa mafanikio pamoja na mashabiki wao kila mwaka,ambapo kwa mwaka huu kuna mikoa kadhaa imeongezeka.
Kupitia kipindi cha XXL Sebastian Maganga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta 2014 amesema mwaka huu kuna mikoa mine imeongezeka lakini kwa utangulizi kwa kanda ya ziwa imeongezeka Kahama na Bukoba.
Fiesta 2014 itaanzia Mwanza August 09 kisha wiki ya pili ni Bukoba ambayo itakua August 15 na Kahama August 17 baada ya hapo ni Musoma August 22 na Fiesta 2014 kwa kanda ya ziwa itamaliziwa Shinyanga Mjini August 24.
SERENGETI 2014 TUPO PAMOJA,SAMBAZA UPENDO..NI SHEEEEDAH.

No comments