Wapalestina wakimbia Gaza kaskazini
Mamia ya Wapalestina wamekuwa wakikimbia sehemu za
kaskazini za Gaza, baada ya Israel kuonya kuwa italenga sehemu hiyo
katika mashambulio yake ya sasa.
Umoja wa Mataifa umenukuliwa ukisema kuwa watu kama 4,000 tayari wameomba hifadhi katika hifadhi ya muda.Wapalestina zaidi ya 160 wameuwawa hadi sasa.
Hamas imerusha makombora zaidi dhidi ya miji ya Israel pamoja na Tel Aviv; hakuna mtu aliyekufa Israel.
Israil ilisema wanajeshi wane walijeruhiwa waliposhambulia eneo ambapo makombora yakirushwa.
Hamas inasema wanajeshi wa Israil hawakuwahi kufika ardhini.
No comments