Watu 29 wauawa katika shambulizi, kenya
Wizara ya maswala ya ndani nchini Kenya inasema kuwa takriban watu thelathini wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makaazi ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa Somali.
Inadaiwa kuwa watu walikuwa wakitizama mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Shambulizi la pili lilitekelezwa karibu na eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika shambulizi jengine mwezi uliopita.
Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo.
No comments