Justin Bieber ahatarisha maisha ya mwanamke mtembea kwa miguu, polisi waingilia kati
Justin Bieber ambaye hivi sasa yuko katika kipindi cha matazamio ameripotiwa kuhatarisha maisha ya watembea kwa miguu katika eneo la Beverly Hills akilazimisha kukwepa foleni.
Mwimbaji huyo anadaiwa kuhama barabara kuu na kuingia kwenye eneo la waenda kwa miguu akiwa katika mwendo kasi kwa lengo la kukwepa foleni.
Kwa mujibu wa TMZ Justin alichepuka na kutaka kumgonga mwanamke mmoja mwenda kwa miguu aliyekuwa katika kibarabara cha waenda kwa miguu.
Msemaji wa polisi katika kitengo cha Beverly Hills aliiambia E! News wanamtaka Justin kufuata sheria za barabarani
No comments