ads

Breaking News

Kanye West afichua kuwa baba yake pia alikuwa Paparazzi, aeleza sababu za kumpiga paparazzi



Kanye West ambaye mwaka jana alikuwa na ugomvi mkubwa na wapiga picha (Paparazzi) na kufikia hatua ya kumshambulia Paparazzi Daniel Ramos katika uwanja wa ndege Los Angeles amefichua kuwa baba yake mzazi aliwahi kuwa paparazzi pia.
Kwa mujibu wa MailOnline ambao wamepata nakala ya discussion  ya maridhiano kati ya Kanye West na mwanasheria wa paparazzi Ramos aitwae Nate Goldberg, rapper huyo alitoa siri hiyo wakati wa maongezi.

Kanye alieleza kuwa wazazi wake hawakumlea kuja kupigana mieleka hadharani na wapiga picha.

“My father was a paparazzo himself. My father was a medical illustrator, a Black Panther, a Christian marriage counsellor. My mother was the first black chair of the English department in Chicago State. They didn't raise me to be out here wrestling with random paparazzi in front of LAX."

Rapper huyo alisikika akieleza kuwa mara nyingi amekuwa akipata msaada kutoka kwa Paparazzi ambao wamekuwa wakimsaidia kuegesha gari lake, kulilinda wakati hayupo na hata kuhakikisha hasumbuliwi na polisi baada ya kuegesha gari lake.

“Kuna watu wema huko nje wanaojaribu kuzilisha familia zao (kupitia upigaji picha) na pia kuna wapumbavu kama huyu jamaa unaemuwakilisha.” Kanye West alimwambia mwanasheria huyo.

No comments