Nick Cannon amtembelea Mariah Carey nyumbani kwake na wamekubaliana haya
Nick Cannon ambaye alitangaza kuwa ametengana na mkewe Mariah Carey tangu miezi mitatu iliyopita amemtembelea mkwewe huyo kwa mara ya kwanza nyumbani kwake New York, Jumatano iliyoita.
Chanzo kiliimbia E!News kuwa Mariah ndiye aliyemuita na kumuomba ruhusa ya kuwatoa nje ya jiji hilo watoto wao mapacha wenye umri wa miaka mitatu, Moroccan na Monroe.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani hapo na kuzungumza, Nick Cannon alimkubalia na kumuomba radhi kwa kutangaza hatua yao ya kutengana bila kumshirikisha.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa wawili hao walikubaliana kuwa tangazo la talaka kati yao litatolewa kwa umma na Mariah Carey mwenyewe na kwamba Nick anatakiwa kuwa kimya kuhusu suala la talaka yao.
Nick Cannon na Mariah Carey walifunga ndoa mwaka 2008 na ndoa yao ilidumu hadi walipotengana miezi mitatu iliyopita baada ya Nick kuwataja wasichana maarufu aliowahi kutoka nao kupitia kipindi cha radio na majina yaliyotajwa ni pamoja na Kim Kardashian.
No comments