ads

Breaking News

Picha 10 za mawe ya Mwanza yalivyoporomoka na kuua ndugu zetu wanne.

Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.45 AM



Screen Shot 2014-08-19 at 9.04.53 AM

Watu wanne wa familia mbiili tofauti wakazi wa mtaa wa Nyerere A, eneo la mabatini jijini Mwanza wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha. 

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza Hassan Maulid amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.

Kaimu kamanda wa jeshi la uokoaji na zimamoto mkoa wa Mwanza inspekta Augustino Magere amewashauri wakazi wa jiji la Mwanza waishio maeneo ya milimani kuchukua tahadhari ili kuepusha maafa kama yaliyojitokeza.
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.00 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.07 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.16 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.46 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.05.53 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.06.00 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.06.09 AM
Screen Shot 2014-08-19 at 9.06.36 AM

No comments