Vodacom Tanzania yaja na Fistula Ice Bucket Challenge
Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge
‘#BongoIce’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula. Hii ni kufuatia kampeni inayoendelea mitandaoni ikijulikana kama #ALSIceBucketChallenge ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake wengi Zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.
Mkurugenzi
wa Vodacom, Rene Meza amekuwa wa kwanza kushiriki kampeni hii na kuwateua Naibu
Waziri wa Mawasiliano Mhe January Makamba, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo
Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel ndugu Sunil Colaso
kushiriki kampeni hii. Fuatilia kupitia:
No comments