ads

Breaking News

Exclusive Pics: Ndoa ya Inspector Haroun yatimiza miaka 10, atoa siri za kudumu kwake


IMG-20140916-WA0015
                             
Ndoa ya Haroun Rashid Kahena aka Inspector Haroun imetimiza miaka 10. Rapper huyo wa ‘Mtoto wa Getu Kali’ alifunga ndoa na mke wake May 5 mwaka 2004.

IMG-20140916-WA0001
Mwaka 2004 ndoa ya Inspector ilipofungwa
Wanandoa hao kwa sasa wana watoto wawili, Nassir na Shadya.
IMG-20140916-WA0004
Mke wa Inspector akiwa na wanae, Shadya na Nassir

“Tulifanya sherehe ndogo ya kifamilia lakini ndani ya mwezi wa kumi mwaka huu tunataka kufanya sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka kumi ya ndoa yetu sababu nataka nisherehekee na fans wangu pamoja na mashibiki wote wa muziki kwa ujumla,” Inspector ameiambia Bongo5. “Nitawaambia rasmi itakuwa wapi, lini na tarehe gani. Nashukuru Mungu kunifikisha hapa na familia yangu pia kutujalia afya njema.”
IMG-20140916-WA0002
Familia yenye furaha: Mke wa Inspector aka Babu akiwa na wanae
IMG-20140916-WA0012
Watoto wa Inspector, Shadya na Nassir

“Siri ya mafanikio yetu kila mmoja kukuubali udhaifu wa mwenzie na kujikinga na skendo pia kudhamiria kuishi ndani ya ndoa na kuhimili misukosuko ya kila aina haijalishi hata nikiyumba kwa kipato huwa tunavumilia na kuchukua kama changamoto za maisha yetu,” amesema Babu.
IMG-20140916-WA0006
Like father like son? Mtoto wa kiume wa Inspector Haroun, Nassir
IMG-20140916-WA0008
Shadya
IMG-20140916-WA0009
Nassir na Shadya

No comments