ads

Breaking News

Linex: 'Wema Kwa Ubaya' ni video ya Bongo Flava iliyomlipa pesa nyingi zaidi Adam Juma tangu aanze production


Mwimbaji kutoka Kigoma, Linex amesema kuwa video ya wimbo wake mpya ‘Wema Kwa Ubaya’ ndio video ambayo imemlipa muongozaji Adam Juma kiasi kikubwa zaidi cha pesa kwa video moja ya wimbo wa Bongo Flava.
Linex ameiambia tovuti ya HII kuwa mheshimiwa Zitto Kabwe aliamua kumpa Adam Juma kiasi cha shilingi Milioni 5 ili kuhakikisha wanapata video bora zaidi.
Kiasi hiki kinazidi mbali kiasi alichowahi kukitaja Adam Juma kuwa hakuna msanii wa Bongo Flava aliyewahi kumlipa zaidi ya milioni 3 na nusu kufanya video moja.
Tulimtafuta Adam, na tumemlipa Adam shilingi milioni 5 kwa lengo la kupata video ambayo ni nzuri, kupata kitu ambacho ni tofauti. Tumemlipa Adam kiasi ambacho hamna msanii yeyote wa Bongo Flava aliwahi kumlipa. Adam juzi kati alisema hakuna msanii yeyote wa Bongo Flava ambaye aliwahi kumlipa zaidi ya shilingi milioni 3 na nusu.”

No comments