Noorah: Tusiseme tunaenda internatioanal wakati hatujajipanga
Rapper wa kundi la Chamber Squad, Noorah aka Babastylez, amedai kuwa haiwezekani kwa wasanii wengi wa Tanzania kufanikisha ndoto yao ya kufanikiwa kimataifa kama wataendelea kufanya muziki kwa kuiga.
Noorah amesema wasanii wengi hawajui dhana nzima ya kwenda international. “Kwasababu wengi wanapenda kukopi kitu fulani ambacho kinafahamika sana sehemu kubwa waweze na wenyewe kupenetrate kuingia huko,”alisema Nooah.
“Kuna sampling na copying. Tuache kukopi, sampling inaruhusiwa ila tuache kukopi, tusample.”
Noorah amedai kuwa wasanii wanatakiwa kufanya utafiti wa kina kufahamu soko la kimataifa linahitaji nini ili waweze kufanikisha ndoto hizo.
No comments