ads

Breaking News

Yanatimia mwezi huu, Barnaba na Fally Ipupa

Barnaba ambaye ameutaja mwaka huu kuwa mwaka wake wa mafanikio zaidi ameelezea mpango wa safari yake kwenda Ufaransa na Marekani mwezi huu.
 msanii huyo amesema kuwa safari yake italenga katika kukamilisha collabo yake na Fally Ipupa pamoja na video lakini pia ataenda New York kwa ajili ya mradi wa Malaria No More.
“Panapomajaliwa katikati ya mwezi ujao naenda Ufaransa. Nikitoka Ufaransa narudi tena New York na baada ya hapo narudi Dar. Kwa ajili ya Hawalade lakini pia kwa ajili ya project nyingine. Kwa sababu mimi pia ni balozi wa malaria no more, kwa hiyo naenda kama balozi ambaye naenda kuchukua elimu kidogo.”
“Lakini Ufaransa naenda kwa ajili ya Fally Ipupa. Naenda kufanya collabo nae na wimbo wangu pia nafanya nae. Huo wimbo ulifanyika ulikuwa nusu hakumaliza. Kwa hiyo inabidi nimfate kule tumalizie kule. Masters nitafanyika kule na video ntafanyia kule panapo majaliwa.”

No comments