Mmiliki wa Facebook amenunua huu upande wa kisiwa cha Hawaii.
Mwaka jana mwenyekiti wa Oracle Larry Ellison alinunua upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa dola milioni 600 ambapo stori nyingine zinasema Zuckerbug nae anaweza akawa na nia ya kuanzisha majengo upande huo wa Lanai baada ya kuonekana na mkewe Priscilla Chan kwenye maeneo hayo.
Haya yatakua maendeleo mengine ya Zuckerberg kwani mwaka 2010 alikodisha jengo lake ambalo lipo karibu na makao makuu ya office za Faceboook na mwaka uliofata aliongeza makazi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 7 huko Palo Alto, California, Marekani ambapo
pia
baada ya muda mfupi alitumia dola milioni 30 kununua nyumba nne ambazo ziliunganishwa na makazi yake ya Palo Alto.
Alivyoulizwa kuhusu ripoti zilizotolewa hivi karibuni kuhusu matumizi
yake ya pesa msemaji wa Facebook alisema ‘Hatuna chochote cha
kusema kuhusu maneno ambayo hayana ukweli ila asante kwa kututafuta’
No comments