ads

Breaking News

AT awataka wasanii kuacha kuwadharau ma-director wa Tanzania

AT SS
Msanii wa muziki wa mduara, AT amechukizwa na baadhi ya wasanii wa Tanzania kuwadharau ma-director wa nyumbani.
Akizunzungumza na Bongo 5 leo, AT amesema wasanii kuendelea kufanya video na waongozaji wa nje ni kuupoteza kabisa muziki wa Tanzania.
“Wasanii wanalaumu sana directors wa Tanzania, wanadiriki kusema kuwa Tanzania hakuna directors, lakini siyo kweli inatakiwa ifikie hatua sisi watanzania tuwe na shukurani kwa hawa directors wetu kwa kutusaidia kufanya video. Directors wa Tanzania hawakuwa na kamera zenye 4K ile ya picha Quality kama anayofanya nayo Godfather, sisi wenyewe tunaenda kufanya video kwa kuomba, mtu ana laki tano anataka video, director hatawezaje kimiliki kamera ya 4K ya thamani ya milioni 60 au 70 , alafu pia watu wanatakiwa kutambua Godfather au director wengine wa nje ya Tanzania, ni vigumu sana kutengeneza video za kibongo, hawatoweza, mimi naongea na kama kuna mtu ananibishia anibishie, director wa nje hawawezi kutengeneza video za kitanzania bali watanzania wenyewe ndo wanaweza kufanya hivyo,” alisema AT.
Pia AT azungumzia kwanini Diamond aliamua kurudia video ya Mdogo Mdogo kwa Adam Juma.
“Siyo Godfather ajaitendea haki ile video kuna vitu fulani viko sawa, imeingia kwenye tuzo tofauti lakini Diamond ameifanya tena remix kwa Adam Juma, kutokana na kwamba Adam ni Mtanzania ambae anaelewa vitu vingi, nini kinatakiwa kifanyike , hata Godfather akija Tanzania kuna video nyingine inabidi amtafute mtu ambae mwenyeji wa kumwelekeza muziki tunaofanya, muziki wa Tanzania ni muziki unaojitegemea, ni vigumu sana mtu kutoka nchi nyingine akaufanya. Kwa mfano leo hii kuna watu wamekimbilia Kenya mwisho wa siku video unakuta amechukua copy and paste, wakati sisi kwetu hatufanyi hivyo, kweli director wetu hawakuwa na kamera kubwa lakini sasa hivi Adam yupo na Red, na yeye anapiga video nzuri tu, Mdogo Mdogo ni nzuri na nikubwa, lakini ili na watanzania waweze kui-support na yeye anatakiwa aweze kupeleka utamaduni wa mtanzania sehemu nyingine anapaswa kurejea na kufanya kitu kizuri zaidi, kwa sababu ile nyimbo ni mchiriku, hakuna dunia nzima mchiriku ni Tanzania , kwahiyo mtu yoyote wa nje ukimpa kufanya video kwajili ya Tanzania atafanya ili kuonyesha mazingira ya kiafrika ambayo siyo kweli kuwa yanafanana. Kama Godfather kafanya kiafrika lakini kafanya kiafrika kusini, hakufanya kiafrika kitanzania inavyotakiwa iwe, kwamfano mimi nichukue nyimbo yangu ya mduara nikafanye na Godfather atakachonifanyia humo ni quality nzuri lakini mwonekano wa matukio ya kiutamaduni yataonekana yaki South, sasa watanzania wengine itakuwa vigumu kuupokea.”

No comments