Jose Chameleone amuomba Diamond Platnumz wafanye collabo
Mtandao wa Bigeye wa Uganda umeripoti kuwa Chameleone amekuwa akiwasiliana na Diamond kwa whatsapp akimuomba waingie studio na kufanya wimbo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo inadaiwa kuwa Diamond amemuomba Mr Mayanja avumilie kidogo mpaka atakapotulia.
Wiki iliyopita Diamond alifanya kazi na msanii mwingine wa kike kutoka Uganda Zari, ambaye alisafiri kutoka Afrika Kusini yaliko makazi yake hadi jijini Dar es salaam kwaajili ya kazi hiyo.
No comments