ads

Breaking News

Jose Chameleone: Sijamuomba collabo Diamond, mimi si msanii mchanga (Exclusive Audio)

10678828_690939977649722_3878316333098729824_nMsanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, amekanusha ripoti zilizoandikwa kwenye mtandao wa BigEye wa Uganda kuwa amemuomba Diamond Platnumz wafanye collabo.

Chameleone amesema kuwa application ya Mziiki ambayo Diamond ni balozi wake wa Tanzania ipo kwenye mazungumzo naye ili kumfanya balozi wake wa Uganda na hivyo ilimuomba afanye wimbo na Diamond kama anthem ya Afrika Mashariki.
“Lakini we talked about business na hatujamalizana nao. Lakini sio eti mimi nimempigia (Diamond) kumuomba tufanye collabo na kitu kama hicho,” amesema Chameleone. “Wale wa Mziiki app ndo wanahitaji mimi na yeye tufanye kazi ya anthem ya Mziiki app. Wanajaribu kuunganisha yeye na mimi tufanye collaboration lakini sio eti mimi nimemuwhatsapp na nimemuomba collaboration , that’s not right,” amesisitiza hitmaker huyo wa Valu Valu.
“Am not at a level of asking for a collaboration from any artist in that manner. Sio kwamba sina heshima yake (Diamond) au kitu kama hicho lakini that’s not the truth, haiwezi kuwa hivyo. I have been doing music for the past 14 years, right? So I am not an upcoming artist.”
Msikilize zaidi hapo chini.

No comments