ads

Breaking News

Mabeste: Bado nipo njia panda

Mabeste akiwa na Joson Gete
Rapper Mabeste amedai kuwa kutokana na kuwa na nyimbo nyingi alizorekodi hadi sasa, yupo njia panda kujua nyimbo gani aachie.
Mabeste amesema kuwa hivi karibuni ataachia wimbo lakini yupo kwenye mchakato wa kupembua ngoma kali zaidi kati ya hizo.
“Ngoma ni nyingi na bado sijachagua ipi iende, kwa sababu bado zinachanganya kiukweli. Kuchagua sahihi ipi iende ipi ibaki,kuna mvutano. Huu mwaka kuna ngoma moja mpya halafu mwakani tutapoanza tutaanza kufungua kwa kuachia tu ngoma. Kila baada ya muda fulani nitakuwa naachia tu ngoma. Kitu kikubwa zaidi nilikaa muda mrefu bila kufanya kazi mfululizo, najua mashabiki wangu kuna vitu vingi wanahitaji. Kwahiyo mwakani kutakuwa na mapinduzi makubwa ya muziki wangu kwa sababu watu wangu wanahitaji vitu vingi zaidi,” amesema Mabesete.

No comments