ads

Breaking News

Mirror kuzindua video mbili kwa mpigo November 30

MirrorMsanii ambaye anasimamiwa na kampuni ya Endless Fame Films ya Wema Sepetu, Mirror anatarajia kuchia video mbili mpya kwa mpigo baada ya kutoonekana kwenye runinga na video mpya toka mwaka huu umeanza.

Kupitia Instagram Endlessfame wameandika:
“Novemba 30 ndani ya New Maisha Club Dar es salaam @mirror26 kutoka @endlessfame atadondosha Video viwili Vipyaaaaa me nawe hatutakiwi kukosa ama vipi??? Nakukumbusha #Team nzima ya @endlessfame itakuwepo pale @wemasepetu @martinkadinda @petitman_wakuache @bestizzo @ricndeki ndaniiiiiiiiii”
Mwezi May, 2014 Mirror alipata nafasi ya kufanya collabo na msanii mkubwa wa Uganda Jose Chameleone wimbo ambao ulirekodiwa AM Records, na katika moja ya mahojiano ya radio aliahidi kuifanyia video kabla haujatoka.
Mwezi August Mirror pia aliahidi kutoa video ya single yake ‘Kolokolo’ ambayo mpaka sasa video hiyo ilikuwa haijatoka.

No comments