ads

Breaking News

Picha za Diamond na Zari the Boss Lady zilizowashtua wengi ni ‘video shoot’ ya wimbo


dz2


Mfanyabiashara na mwimbaji mrembo wa Uganda, Zari the Boss Lady na Diamond Platnumz waliingia kwenye headlines weekend iliyopita baada ya picha zao wakiwa kwenye faragha kama wapenzi kuzua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.
dzHata Hivyo Zari hakuchukua muda mrefu na kuamua kutumia Instagram kufumbua fumbo hilo kwa kuweka wazi kuwa ameshirikiana na Diamond katika wimbo wake mpya.
Zari ameuambia mtandao wa Big Eye wa Uganda kuwa picha zilizosambaa ni sehemu ya video shoot ya wimbo aliofanya na hit maker wa Number 1.
Wimbo huo unatarajiwa kutoka December 18 wakati wa party ya Zari ‘All white Ciroc party’ itakayofanyika kwenye Club Guvnor nchini Uganda.
Kitu ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu ni kuwa , Zari ni muimbaji lakini alikuwa ameweka pembeni muziki kwa muda, na sasa ameamua kurejea.

No comments