ads

Breaking News

Polisi wazuia video shoot ya rapper Tyga baada mashabiki zaidi ya 1,000 wasiohusika kujitokeza location

Tyga vid
Polisi wa Los Angeles, Marekani jana Nov 11 walilazimika kuingilia kati na kuzuia uchukuaji wa video ya mpya ya Tyga, baada ya mashabiki zaidi ya 1,000 ambao wasiohusika na video hiyo kukusanyika eneo ilipokuwa ikifanyika.

Kwa mujibu wa TMZ, mashabiki hao ambao walikuwa hawahisiki kabisa na video hiyo walikusanyika baada ya kugundua kuwa Tyga anashoot video eneo hilo.
Inadaiwa polisi walilazimika kusimamisha zoezi za video kwa sababu za kiusalama, lakini hakuna mtu yeyote aliyewekwa chini ya ulinzi.
Jumatatu Tyga pia alikamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha gari kwa vurugu wakati akiendelea kushoot video hiyo

No comments