ads

Breaking News

Weusi waahirisha show ya Mbeya kufuatia kifo cha Geez Mabovu


Weusi wakifanya yao
Weusi wamethibitisha  kuwa wameahirisha show yao ya Funga Mwaka iliyokuwa ifanyike jijini Mbeya Ijumaa hii kufuatia kifo cha rapper Geez Mabovu kilichotokea Jumatano jioni.
Joh Makini amesema Geez alikuwa kama mtu wa familia yao.
“Kusema na ukweli hatutaweza kufanya show ya Mbeya,” Joh Makini ameimbia Bongo5 kwa huzuni. “Ni kwasababu Geez ni mshikaji wetu, he is part of the family. For the love of hip hop and respect, hatuwezi kufanya.”
Geez amewahi kumshirikisha Joh Makini kwenye nyimbo zaidi ya tatu na walikuwa na uhusiano wa karibu.

No comments