ads

Breaking News

Cheki mavazi aliyovaa Nazizi kwenye kolabo hii mpya na TID…



nazizi 
‘Watasema Sana’ ni moja kati ya  hitsingle zilizowahi kutokea kwenye historia ya Bongofleva, ilimshika kila mtu aliyekuwa na mapenzi na muziki huu ambapo wahusika wakuu walioifanya hitsingle hiyo ni wakali kutoka Afrika Mashariki, Nazizi kutoka Kenya na TID kutoka Tanzania, hakika walifanya kazi nzuri iliyofanikiwa kupenya vizuri kwenye masikio ya wana Afrika Mashariki.
Taarifa ikufikie kwamba wakali hao wameirudia historia hiyo mwaka huu 2014 kwa kurudi tena studio kufanya kazi nyingine, TID na Nazizi kwenye hii nyingine inayoitwa ‘Pressure’,video imeongozwa na Cream Vision mavazi ya Nazizi yamezoeleka kwamba ni yale ambayo huwa yanavaliwa na wanaume lakini humu hali iko tofauti, unaweza kupata picha namna anavyoonekana ndani ya gauni?
Bonyeza play kutazama video hii.

No comments