ads

Breaking News

August Alsina kuungana na Chris Brown kwenye ziara yake Afrika Kusini mwezi April

CA
Mwimbaji wa R&B, August Alsina ataungana na Chris Brown kwenye ziara yake “X Live Tour” nchini Afrika Kusini mwezi April mwaka huu.

Taarifa ya Breezy kwenda nchini Afrika Kusini kutumbuiza ikiwa ni mara yake ya pili, ilitangwazwa mwishoni mwa mwaka jana.
Alsina ameshirikiana na Brown kwenye remix ya wimbo wake “I Luv This Sh*t” ambao waliutumbuiza pamoja kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za 2014 BET wakiwa na Trey Songz.
Breezy na timu yake wanatarajiwa kufanya show mbili nchini humo. Ya kwanza ikiwa ni April 2 jijini Johannesburg, ikifuatiwa na Durban, April 4.
Show hizo ni sehemu ya ziara ya album ya X ya Chris Brown ambayo atazunguka katika nchi mbalimbali.

No comments