Polisi walikuta dawa za kulevya nyumbani kwa mtoto wa Whitney Houston, Bobbi Kristina
Familia ya mtoto wa
kike wa marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina imethibitisha kuwa
polisi walikuta dawa za kulevya nyumbani kwake baada ya kurudi kwa mara
ya pili kufanya ukaguzi, TMZ imeripoti.
Binti huyo mwenye miaka 21 alikutwa bafuni kwenye ‘bathtub’ Jumamosi iliyopita akiwa amepoteza fahamu.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, siku moja kabla ya tukio hilo Kristina alikuwa na rafiki yake ambaye aliwahi kutuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Ripoti ya polisi inadai kwamba Maxwell Byron Lomas, ambaye alikuwa na Bobbi Brown siku aliyokutwa amepoteza fahamu bafuni kwenye ‘bath tub’, aliwahi kukamatwa mwezi mmoja uliopita kwa kusambaza dawa za kulevya na kuwekwa chini ya ulinzi January 14 na baadae kuachiwa kwa dhamana, kwa mujibu wa Fulton County Jail records.
Katika hatua nyingine, Bobbi Kristina amehamishiwa kwenye hospitali nyingine iitwayo Emory University Hospital iliyoko Atlanta, GA inayosifika kwa matibabu bora zaidi ya mishipa ya fahamu, TMZ imeripoti. Toka siku ya Jumamosi alikuwa katika hospitali ya North Fulton Hospital iliyoko karibu na nyumbani kwake huko Roswell, GA.

No comments