Jaguar apewa ‘shavu nono’ na Rais Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemteua Jaguar kuingia kwenye bodi ya mamlaka NACADA inayohusika na kampeni dhidi ya matumizi ya pombe na dawa za kulevya ya nchini humo.
Jaguar amechaguliwa katika nafasi hiyo na maafisa wengine 302 kutokana na hekima, uzoefu, ujuzi, nguvu, ubunifu na kusaidia kundi la vijana katika jamii.
Uteuzi huo ulitangazwa kupitia tangazo gazetini April 27.
Hata hivyo wengi wanahisi Jaguar amepewa shavu hilo kutokana na ukaribu na urafiki mkubwa alionao na Uhuru Kenyatta.
No comments