Mohombi, Alaine waitafuta collabo na Diamond Platnumz
Diamond Platnumz ni msanii anayewindwa kwa udi na uvumba na wasanii wa kimataifa kwaajili ya kufanya naye collabo.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM wiki iliyopita, Diamond alidai kuwa ana orodha ndefu ya wasanii wa nchi mbalimbali wanaopenda kumshirikisha kwenye ngoma zao.
“Nikikutajia collabo ambazo mimi nimeombwa – nimeombwa collabo mpaka na Mohombi, Alaine, wasanii wengi sana wa nje na wa ndani, wengi wanataka kufanya nyimbo zao wanishirikishe mimi,” alisema staa huyo.
Akizungumzia pia collabo yake na Bracket, Diamond alisema Tiwa Savage alitaka kuwepo kwenye wimbo huo kwasababu yake yeye.
“Tiwa Savage baada ya kusikia kuna Diamond katika hiyo nyimbo akaomba awepo katika nyimbo,” alisema.
Diamond Platnumz ni msanii anayewindwa kwa udi na uvumba na wasanii wa kimataifa kwaajili ya kufanya naye collabo.
No comments