Video: Wizkid afunika alipotumbuiza na Chris Brown huko Afrika Kusini, waperform collabo yao mpya kwa mara ya kwanza
Weekend iliyopita muimbaji wa R&B Chris Brown kutoka Marekani alifanya show ya ‘X Tour’ nchini Afrika Kusini, na staa wa Nigeria Wizkid alipata nafasi ya kutumbuiza naye kwenye show ya kwanza iliyofanyika Durban.
Staa huyo wa Nigeria aliperform kwa mara ya kwanza collabo mpya na Chris Brown ‘African Bad Girl’.
Kupitia Instagram Wizkid alipost vipande vya video ya show hiyo na kuandika: “We performed the song for the first time! @chrisbrownofficial x Wizkid!! 2015 alive!! Song nd video soon!”
Kipande kingine cha video kinamuonesha Wizkid akiperform hit yake ya “Show You The Money” huku Chris Brown akigeuka kuwa dancer wake na kusababisha shangwe nyingi kutoka kutoka kwa maelfu ya mashabiki waliohudhuria show hiyo.
Kwenye picha nyingine aliyopiga na Breezy aliandika:
“Durban was mad trill!! @chrisbrownofficial brother 4 life!! Back in joBurg!! Tonight we go all the way up!”
No comments