ads

Breaking News

Nipo kwenye mchakato wa kufanya kazi na Wizkid na D’Banj – Nay Wa Mitego


nnnay

Nay Wa Mitego ameweka wazi mipango yake ya kuanza kujitangaza kimataifa kwa kuwashirikisha wasanii wa nje.
Nay ambaye hivi karibuni ameachia collabo yake na Diamond ‘Mapenzi au Pesa’, amesema tayari ameshafanya collabo na msanii wa Nigeria aitwaye Runtown, na yuko kwenye mchakato ya kufanya collabo na masuperstar wa Nigeria, Wizkid na D’Banj.
“Nimeshafanya kazi na Runtown, this time Wizkid na D’Banj ni watu ambao niko kwenye process hizo kuhakikisha ndo mtu ambaye atakayefata kufanya naye.” Alisema Nay kupitia The Sporah Show.
Alipoulizwa kuhusu wasanii wa Tanzania kuiga muziki wa Nigeria:
“Muziki wetu kama umekuwa sasa tunashare vitu flani. Biashara ndio inatupeleka huko, no wayout inamaana ukipingana nayo utakuwa nje ya mstari tukubali tukatae, biashara ndo iko hivyo ikibadilika tutabadilika.”

No comments