Ice Cube, Nicki Minaj, Eve, Common waigiza kwenye filamu ya Barbershop 3 (Video)
Ice Cube anatarajia kuileta awamu ya tatu ya filamu yake ya Barbershop.
Rapper na muigizaji huyo ameonesha video ya behind-the-scenes ambapo anarejea tena kwenye Barbershop ya Calvin ya Chicago.
Mastaa wengine watakaoonekana kwenye filamu hiyo ni Nicki Minaj, Anthony Anderson, Eve, Common, Cedric the Entertaine na Regina Hall.
Filamu zilizopita za Barbershop (2002) na Barbershop 2: Back in Business (2004) kwa pamoja ziliingiza dola milioni 140.
Barbershop 3 itaingia kwenye majumba ya sinema mapema mwaka 2016.
No comments