Lil Wayne aachia album yake mpya ‘Free Weezy Album’ kupitia Tidal
Baada ya Lil Wayne kutangaza kuwa amesaini deal na Jay Z hivi karibuni, rapper huyo wa Young Money ameachia album yake, ‘Free Weezy Album’ kupitia mtandao wa Tidal.
Album hiyo FWA imetoka leo Jumamosi, July 4.
Wasanii walioshirikishwa kwenye album hiyo ni Wiz Khalifa, Jake Troth, HoodyBaby, Cory Gunz, CAPO, Junior Red, Bibi Bourelly, Euro na Young Jeezy.
‘Glory’ ndio wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo yenye nyimbo 15, ambao pia Weezy aliuachia exclusive kupitia Tidal mwezi uliopita.
Usikilize ‘Glory’ hapa chini
No comments