Victoria Lukuba akitoa Shukrani
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na majaji Pale Nyumbani Park Kihonda
Msimu wa Serengeti Fiesta 2014 Unaoendelea sasa kama kawaida unaambata na kusaka vipaji kwa wasanii chipukizi. Kwa kila mkoa linapofanyika tamasha hutanguliwa na shindano hilo ambalo kwamwaka huu kumekuwa na mabadiliko ya kuhusisha jinsia ya kike tu.
Victoria Lukuba akiwa na majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Producer Vennt Skillz toka kwanza Records, Dicson George Clouds TV na peace toka Planet Fm
Jumapili iliyopita tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lilifanyika mkoani Morogoro katika uwanja wa Jamhuri stadium ambapo shindano la kumsaka Super Nyota Diva limefanyika katika ukumbi wa Nyumbani Park $ Samaki Spot Kihonda Bima. Katika shindano hili lililoshirikisha washiriki zaidi ya 16 mshindi ambaye ndiye atakayeiwakilisha Morogoro ni Victoria Sostheness Lukuba (21 yrs)
Victoria Lukuba mara baada ya kutangazwa mshindi
No comments