ads

Breaking News

Kabla ya Kanye West kulikuwa na hawa 9 kwenye maisha ya Kim Kardashian…(Pichaz)!

Kim Kardashian ni staa wa Tv na Social Media pia ni actress, mfanyabiashara, model na mama aliyepata attention ya kwanza na media kupitia urafiki wake na model Paris Hilton lakini badaae umaarufu wake ukaja kukua baada ya ex boyfriend wake Raj J kuvujisha mkanda wa mapenzi kati yao mwaka 2007.
Mwishoni mwa mwaka 2007 Kim na familia yake waliaanza kuonekana kwenye Tv kupitia kipindi chao cha ‘Keeping Up With The Kardashias’ na kufikia mwaka 2010 Kim alikuwa staa pekee wa reality Tv shows anaelipwa dola million 6 (Billion 12) kwa mwaka.
kimkim
Kim Kardashian.
Kuna mengi sana tunayasikia kuhusu staa huyu, lakini unajua ni idadi ngapi ya mastaa waliowahi kuwa kwenye mahusiano na Kim Kadarshian? wangapi waliowahi kufunga nae ndoa? Nimefanikiwa kuwakusanya mastaa 9 waliowahi kuwa na Kim kimapenzi na wengine walifanikiwa hata kuwa nae kwenye ndoa…
kim1
Kim Kardashian na Producer Damon Thomas waliwahi kuwa kwenye ndoa kwa miaka 4 (2000 mpaka 2004) baada ya hapo wakaachana.
kim2
Producer Ray J Norwood mdogo wa superstaa Brandy Norwood alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Kim mwaka 2005 hadi 2006.
kim3
Baada ya kuachana na Jesica Simpson mwaka 2006, muigizaji Nick Lachey aliingia kwenye mahusiano na Kim Kardashian na kuachana ndani ya mwaka huo huo.
kim4
Baada ya kuachana na Nick Lachey mwaka 2006, safari ya mapenzi iliendelea na Nick Cannon.
kim5
Mapenzi na Nick Cannon yalivyoisha mwaka 2009, Kim Kardashian aliamua kuanza ukurasa mpya na staa wa basketball Reggie Bush mwaka 2010.
kim6
Baada ya kushindwana na Reggie Bush, Kim Kadarshian alitafuta pumziko kwa Miles Austin mwaka huo huo wa 2010.
kim7
Cabriel Aubry alianza ukurasa mpya na Kim Kardashian mwaka 2010 baada ya kutengana na mpenzi wake wa muda mrefu; Halle Berry.
kim8
Baada ya miezi michache Kim Kardashian alianza kuonekana na staa wa NBA Kris Humphries na mwaka 2011 kaka huyo alimvesha Kim pete ya uchumba na ndoa ikafungwa mwezi wa 8 mwaka huo huo lakini wawili hao walipeana talaka baada miezi 4 ya ndoa.
kim9
Mwaka 2012 ikawa zamu ya Kanye West , baada ya mwaka mmoja wa mahusiano Kim alitangaza kuwa anategemea kupata mtoto wake wa kwanza na rapper Kanye na mwaka 2014 mwezi wa May wawili hao walifunga pingu za maisha!

No comments