Ajali ya ndege yawauwa wanne Kenya
Watu wanne akiwemo Rubani wa
ndege moja ya mizigo, wamefari dunia baada ya ndege walimokuwemo
kuanguka mapema leo asubuhi katika eneo la Utawala- Embakasi jijini
Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu Nchini
Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba SHEHENA ya Miraa ama milungi kuelekea Mogadishu Nchini Somalia.
Barabara ya Estern Bypass jijini Nairobi imefungwa kwa muda huku msongamano mkubwa wa magari ukishuhudiwa.
No comments