DAKTARI NA MGONJWA WA MENO WAFUMANIWA WAKIJIANDAA KUFANYA MAPENZI NDANI YA HOSPITALI MOJA TEMEKE JIJINI DAR
Daktari
wa meno aliyejulikana kwa jina la Dokta Ngariba (54), amejikuta ndani ya janga
la tuhuma za ngono baada ya wapiga picha za Udaku kunasa sakata lake na
mwanamke aliyedai ni mgonjwa wa jino aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamida
(20).
Tukio hilo la kushangaza lilijiri
Juni 9, mwaka huu ndani ya Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Temeke
kilichopo Kigamboni jijini Dar ambapo timbwili hilo lilitokea.
Ilikuwa wakati mwandishi
akizunguka katika Jiji la Dar es Salaam kusaka matukio ndipo alipopita
nje ya kituo hicho alisikia sekeseke kutokea kwenye chumba ambacho baadaye
kilibainika na cha kung’olea meno.
Katika uchunguzi na ufuatiliaji ,
mgonjwa huyo alisikika akidai kwa polisi waliofika kutuliza sakata kuwa,
alijihimu kwenye kituo hicho kwa lengo la kung’oa jino lakini katika hali
ambayo hakuitarajia daktari huyo alimtaka kimapenzi naye akajikuta akitumbukia.
“Mimi nimekuja kung’oa jino,
linaniuma leo sijui siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka
kimapenzi. Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria,” alisema mwanamke huyo ambaye alikutwa ameshavua dera.
Daktari akijitetea.....
Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha
mgonjwa wake huyo atambe kiasi hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa, alimpokea
mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha kung’olea
meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha kumvua na yeye shati
na baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.
Akiendelea kuzungumza mbele ya
Polisi wa Kituo cha Kigamboni waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha
matibabu ya meno, daktari huyo alisema:
“Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua
ni mgonjwa anataka tiba ya kung’olewa jino.
“Sasa nikiwa katika maandalizi
ghafla nikamwona anavua nguo na kisha akanivaa mimi na kuanza kunivua shati.
Nashangaa sana anaposema nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani.”
Baada ya maelezo ya Dokta Ngariba,
mwandishi alikuwa na maswali yake lakini hakupewa nafasi ya kuyauliza kwa
vile alidandia ugomvi.
Swali la kwanza; kama kweli Dokta Ngariba alivamiwa na kuvuliwa nguo na
mgonjwa huyo, alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa watumishi wenzake?
Swali la pili; mpaka mgonjwa anajivua nguo zake kisha kumvua yeye shati na
baadaye kuelekea kwenye fraizi ya suruali, yeye alikuwa anawaza nini
akizingatia ni mgonjwa wa meno?
Wakielekea kituo cha
Polisi Kigamboni.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
No comments