Huyu ndio mwigizaji wa filamu ya Harry Potter aliyekutwa amekufa.
Mwigizaji raia wa Uingereza aliyecheza series za Harry Potter amekutwa amekufa jijini California, kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo.
Dave Legeno, mwenye umri wa miaka 50, alikutwa akiwa amepoteza maisha siku ya Jumapili na mwili wake kuchukuliwa na helicopter.
Hakukuwa na alama zozote za uhalifu katika eneo alipokutwa na inaaminiwa kuwa alipoteza maisha kutokana na joto kwa mujibu wa uchunguzi wa awali.
Amecheza katika series tatu za filamu ya Harry Potter ikiwemo Deathly Hallows.
No comments