Israel yaanza kushambilia Gaza tena
Israel imeanza tena kushambulia Gaza ikidai kuwa Hamas inaishambulia licha ya mkataba wa kusitisha vita
Awali Israel ilikubali kusitisha vita kufuatia pendekezo la Misri kwa pande zote mbili kusitisha vita Jumanne asubuhi.
Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu 192 wameuawa katika mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku nane zilizopita ili kukomesha wapiganaji wa Hamas kuusha makombora nchini Israel.
Raia wanne wa Israel wamejeruhiwa vibaya tangu mashambulizi hayo kuanza , lakini hakuna taarfa zozote za vifo.
Mashambulizi ya hivi punde yamepiga maeneo mawili katika ukanda wa Gaza.
Kundi la Hamas lilisema kuwa hawajapokea pendekezo lolote la kusitisha mashambulizi.
Aliongeza kwamba Hamas inahitaji masharti yake yote kukubaliwa kabla ya kukubali kusitisha vita.
Idara ya usalama nchini Israel imekubali mapendekezo hayo lakini ikasisitiza kuwa itaendelea kushambulia Gaza ikiwa Hamas watasitisha kusidhambulia kwa roketi.
No comments