MCHUNGAJI GWAJIMA KAIMBIA NCHINI
MBASHA akiwa na Mkewe FLORA
Kufuatia sakata la Flora Mbasha na mumewe likumuhusisha moja moja kiongozi wa kiroho Mchungaji Gwajima, habari tulizozipata ni kwamba mchungaji huyo amekimbia nchi….
Habari
toka chanzo cha kuaminika kilichopo ndani ya kanisa la
mchungaji huyo ni kuwa Gwajima hivi sasa ameshauza karibia
robo tatu ya mali zake na kwamba moja kati ya magari yake
ya kifahari huenda likanunuliwa na mwanamuziki Diamond.“Jamaa
hivi tunavyoongea anaweza akawa ameshatoroka tayari, maana hili
sakata limeanza kumwendea hovyo na wiki iliyopita kuna madalali
walikuja hapa wakiitaka gari yake aina ya Hammer, wakidai kuwa
inataka kununuliwa na mwanamuziki Diamond,” kilisema chanzo cha
habari hii.
Kikaendelea
kumwaga data kuwa karibu wiki zima lililopita mchungaji huyo
alikuwa kwenye mipango ya kuuza baadhi ya nyumba zake na
kwamba hata familia yake hivi sasa haiko kwenye makazi yake
anayoishi siku zote…“Hata
familia yake sijaiona karibu wiki mbili hapa kanisani na
taarifa tulizonazo karibu waumini wengi tu ni kwamba jamaa
anataka kuhama nchi lakini hatujui ni nchi gani anayotaka kwenda
kufanya makazi yake tena ya kudumu,” alisema.Habari
hizo zinadai kuwa baadhi ya waumini wamepanga kugawana mali
kadhaa za kanisa pamoja na za Gwajima mwenyewe endapo
itagundukia kuwa ametoroka kweli….“Kuna
baadhi ya waumini wamekerwa sana na hii skendo ya Flora
Mbasha, wamekuwa wakijiapiza kwamba hata zile mali zake ni
halali yao kwani zinatokana na sadaka wanazotoa kila siku,
inasikitisha sana kwa kweli.” alisema mtoa habai hii.Inasemekana
kuwa mchungaji Gwajima amepanga kuwaaga waumini wake kama vile
anakwenda kueneza neno katika mataifa mengine, lakini ukweli ni
kwamba anataka kuondoka ili kukwepa aibu kutokana na mambo
yanayoendelea…
“Jamaa
yupo kwenye hali ngumu, hii ishu ya Flora Mbasha imemuweka
katika wakati mgumu sana kwa sababu amekuwa akinyooshewa vidole
sana, na kuna baadhi ya wazee wamekuwa wakimtaka atoe tamko
rasmi ili kukwepa hiki kikombe cha aibu,” kilisema chanzo hicho.
Mwandishi
alimpigia simu Gwajima lakini simu yake haikupatikana, na hata
Diamond naye alipopigiwa simu ili kujua kama kweli anataka
kununua gari la Gwajima, simu yake iliita bila kupokelewa na
hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu kitu
No comments