ads

Breaking News

Wakamatwa wakiuza viungo vya binadamu

Kamishna wa jeshi Polisi katika mji wa Kwara nchini Nigeria Mr Ambrose Aisabor,amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili miongoni mwa wengine, waliokuwa wakijishughulisha na uuzaji wa viungo vya binadamu.
Akihojiwa na waandishi wa habari kamishna Ambrose alisema watuhumiwa Amos Kareem na Abubakar Ladan,walikamatwa kufuatia msako mkali ulio endeshwa na jeshi hilo na baada ya kuhojiwa kwa masaa kadhaa watuhumiwa walikiri kuhusika na tukio hilo.

Aidha kamishna Ambrose amesisitiza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wengine

No comments