Bob Junior Azungumzia Wimbo Wake Na Dr Jose Chameleone.
Msanii Bob Junior Wa Sharobaro Records ameongea asubuhi ya August 5 2014 nakuthibitisha kuwa amefanya kazi na Msanii mkubwa Afrika Mashariki Dr Jose Chameleone. Bob Junior anasema..
“Nimerekodi kazi na Chameleone,itafanyiwa final mixing nchini Uganda na producer wake, jina la wimbo sita weka wazi sasa ila wimbo nimeandika sehemu yangu na Chameleone ameandika yake,Utatoka mwezi wa kumi mwaka huu, Naenda Uganda wiki ijayo kuikamilisha kazi na sijamlipa Chameleone pesa yeyote ila tutafanya kazi kwa mkataba kuanzia sasa, sisi ni Business Partners” Alisema Bob Junior
Video mpya ya Bob Junior “Bolingo” inatoka ijumaa ya tarehe 8,8,2014 na utaitazama hapa
No comments