MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS FM ASABABISHA AJALI NA KUKIMBIA, POLISI WALA NAYE SAHANI MOJA HADI WAKAMDAKA
Mtangazaji Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,
Ephrahim Kibonde amedhibitiwa na Askari wa Usalama barabarani wakati
alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema leo asubuhi jijini Dar es
salaam.
Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi ya leo eneo la Makumbusho,
ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa
nyuma.
Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona
hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila
kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki
katumia gari lililogongwa kumfukuzia.
Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.
Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.
Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki
akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza
kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao
aliopo ndani ya Gari hiyo.
Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na
Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na
ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na
kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni!
Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye
kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako
yupo mpaka sasa.
Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.
No comments