Q-Jay kusikika tena kwenye bongo fleva baada ya ukimya mrefu toka aokoke
Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye muziki huo katika wimbo mpya.
Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q-Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’, ambao ni wa kuhamasisha amani.
JIKUMBUSHE NA HII sifai q jay ft joslin
No comments