WHAT LOVE!!!! DAHHH:Msichana wa kihindi aachana na familia yake tajiri na kuhamia kijijini kwa kijana Mkenya
Huko Kenya, kumeripotiwa tukio halisi lililovuta hisia za wengi na kuzungumzwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, ambapo msichana wa kihindi ameamua kuachana na familia yake tajiri na kuambatana na kijana wa Kenya aliyezama nae kwenye vilindi vya mahaba.
Msichana huyo wa kihidi anaifahamika kwa jina la Sarika Patel, ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu, Timothy Khamala uamuzi ambao ni nadra kutokana na mila na desturi za kihindi na kilichoshangaza zaidi ni kuwa wawili hao wanaishi maisha duni kijijini.
Kwa Sarika, maisha ya umasikini sio kikwazo cha kulipata penzi la kijana Timothy aliyenasa kwenye penzi lake.
Safari ya penzi la Sarika na Timothy ilianzia nyumbani kwao Sarika ambapo kijana Timothy alikuwa akifanya kazi na baadae kutimuliwa kwa kudhaniwa kuwa ana uhusiano na princess wa jengo hilo (Sirika) jambo ambalo lilikuwa kweli.
Ingawa wawili hao wamejitoa na kuendelea kuishi pamoja licha kukiri kuwa wanakabiriwa na changamoto kubwa ya kutengwa na jamii ya upande wa familia ya kwao Sarika kwa kuwa kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwa mujibu wa mila na desturi zao, ambapo watu wa jamii sawa ndio wanaooana.
Hata hivyo, Sarika ameelezea msimamo wake kuwa utofauti wa rangi na tamaduni au ufukara wake hauwezi kumtenga na mpenzi wake wa dhati Timothy.
Mapenzi sio pesa, mapenzi ni moyo.
No comments