Barnaba aeleza kwanini hutumia muda mfupi kuandika nyimbo zake
Barnaba amesema kuandika nyimbo zake kwa muda mfupi tu ni kipaji alichopewa na Mungu. humchukua dakika 30 tu kuandika nyimbo zake au za wasanii wengine.
“Unajua nyimbo zangu huwa naandika kwa kutumia dakika chache sana kama wimbo wangu huu mpya niliandika kwa kutumia dakika 30 lakini zingine zote huwa ni kuanzia dakika 25,30, hadi 40 inatagemea na mzuka ukoje siku hiyo,” amesema. “Naona hiki nikipaji ambacho Mungu amenipa. Kwahiyo na mimi nawapa mashabiki wangu nyimbo nzuri kama hizo. Unajua hadi sasa hivi nimeshaandika nyimbo nyingi sana, nimeandika hadi album za watu wengine na bado nyimbo za Gospel, zipo nilizoandika. Namshukuru aisee sana Mungu kwa kunipa hiki kipaji. Wasanii wengi nimewaandikia sipendi kuwataja napenda wenyewe waje kusema.”
Kuhusu kazi mpya, Barnaba amesema: Sasa hivi nakuja na ngoma ambayo sio ya kukimbia sana ipo kama RnB yaani wimbo fulani hivi upo katika mahadhi hayo. Lakini mashabiki wasubiri ndo watauelewa vizuri. Pia najiandaa kushoot video ya wimbo huo ambao ndo utakuwa wimbo wangu wa kwanza kumshirikisha mwana hip hop humo ndani. Nimemshirikisha Mr Blue na video nafanya na Nick Dizzo, ngoma inaitwa “Marry Me” producer ni Ema the Boy na mimi mwenyewe.”
Barnaba ameongeza kuwa atatoa album iitwayo ‘Nimeona’ atakayowashirisha wasanii mbalimbali wakiwemo wa nje ya nchi.

No comments