ads

Breaking News

Country Boy kuja na filamu ‘Money, Power, Respect’, Young D na Dogo Janja wamo

COUNTRY-BOY-YOUNG-DEE
Rapper Country Boy anatarajia kufanya filamu iitwayo ‘Money, Power, Respect’ ambayo watakuwemo pia wasanii wengine kama, Young D Janjaro.

Country Boy ameshaandika script za filamu mbalimbali na anachosubiria ni kutafuta kampuni atakayofanya nayo kazi.
“Kuna project za movie ambazo tumekaa na watu wangu wa karibu kabisa, moja inaitwa Money, Power, Respect. Ni movie ambayo itakuwa inahusu maisha ya wasanii jinsi wanavyohustle, jinsi wanavyotafuta pesa, heshima yao! Kwahiyo ni Money, Power, Respect kwamba inazungumzia pesa, nguvu na heshima. Script ipo tayari ni hii ambayo itangumzia young rapper. Ila mpaka sasa hivi bado sijapata mtu wa kunisupport ili nifanikishe hili kwa sababu movie ni budget. Kwahiyo nitaigiza mimi mwenyewe na baadhi ya wasanii wenzangu wa karibu ambao nawafikiria kuwaweka pia. Young Dee pia atahusika, akina Dogo Janja, yaani Young rapper wote, akina M-Rap. Kwahiyo kama ikitokea uhakika wa kuifanya hiyo movie tutaifanya.”
Country Boy amedai kuwa alianza kuigiza kabla hata ya kufahamika kwenye muziki.
“Mimi nimeshaigizaigiza sana tangu niko mdogo lakini muziki ndo ikawa choice yangu kubwa,” amesema. “Sikubase sana kwenye filamu kwa sababu maisha yangu yamekulia kwenye maisha ya muziki. School ndo nilikuwa nimebase sana kwenye haya masuala ya kuigiza. Kwahiyo nikajiona nina uwezo mkubwa kwa sababu unajua ukiwa na kipaji cha kuimba basi hata kuigiza pia unaweza kwa sababu ukiweza kumface mtu zaidi ya mmoja ukiwa unafanya show basi unaweza hata ukaiface kamera moja. Kwahiyo ni kitu ambacho nina uwezo nacho ila tunategemea tukipata huyo mtu basi mambo yatakuwa oya oya.”

No comments